Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Maelfu ya Wananchi wa Bahrain waliandamana leo kutangaza kuwa wapo pamoja na Madaktari walotiwa mbaroni na utawala wa Alikhalifa Nchini humo.
Kutokana na hali ya Nchi hiyo, Wananchi walieleza kuwa siku ya Ijumaa itakuwa ni siku ya kuhami madaktari na kufahamika hatima ya watu 13 waloshikwa nchini humo katika Mji Mkuu wa Bahrain Manamah, na jina la Ijumaa hii itakuwa ni: HAKI KUAINISHA HATIMA YA WATU 13.
Kwa upande mwengine Sheikh Ally Salman Katibu Mkuu wa Chama cha Al Wafaq Bahrain katika safari yake ya Misri alieleza kuwa Chama cheke hakipo kwa ajili ya kugawanya nchi kama inavyodaiwa na utawala wa Alikhalifa Bahrain, na sisi hatufanyi mambo yetu kwa kuathiriwa na Nchi zingine.
Sheikh Ally Salman katika safari yake ya Misri, na alizungumza na mmoja kati ya Viongozi wa Chama cha Al Wafd Cairo akisema: Utawala wa Bahrain watuhumu wapinzani kuwa wasaidiwa na nchi za nje, madai haya ni ya madikteta yote Duniani hawaitakidi mabadiliko na hutumia kauli hiyo kwa wapinzani.
Chama cha Al Wafd Misri kilieleza kuwa madai ya wapinzani wa Bahrain ni sahihi na yapo sambamba na demokrasia na si kama inavyodaiwa.